DAUDA KIFUNGO PALE PALE

Kamati ya maadili ya TFF imeamua kutupilia mbali maombi ya mjumbe wa DRFA aliyefungiwa na TFF, Bw Shafii Dauda hivyo ataendelea kutumikia adhabu hiyo.

Shafii aliomba shauri lake kusikilizwa tena ili haki itendeke pamoja na kuomba kamati imuondolee adhabu ya kufungiwa na faini lakini amegonga mwamba.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kamati ya maadili Mwita Waisaka, Shafii Dauda alishindwa kuhudhuria kikao cha kamati hiyo na pia ameshindwa kutekeleza maamuzi ya kufungiwa.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.