Mwandishi wa Habari TBC afariki Dunia

Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema kifo cha Mwandishi wa Habari wa TBC Joachim Kapembe aliyefariki jana akiwa Mlimani Kilimanjaro kimetokana na ajali ya Baiskeli na sio madhara ya kupanda Mlima Kilimanjaro. 

“Nimesikitishwa sana na kifo cha Rafiki yangu Joachim Kapembe tuliyekuwa nae kwenye safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro, Kapembe amefariki kwa ajali ya baiskeli wakati akitoka katika kambi ya Kibo kuelekea kambi ya Horombo baada ya kupanda mlima hadi kufika kileleni kwa mafanikio na ni mmoja wa Watu ambao hawakupatwa na madhara ya kupanda mlima (mountain sickness)” ——— Msigwa.

“Baada ya kufanikiwa kufika kileleni Kilimanjaro na kushuka, Watu wote tulifika kambi ya Kibo ambako tulipaswa kuendelea kwenda kambi Horombo, wachache waliamua kutumia baiskeli badala ya kutembea kwa miguu akiwemo Joachim Kapembe bahati mbaya akiwa anateremka mteremko wa kutoka Kibo ndipo akapata ajali iliyosababisha apoteze maisha”

“Natoa pole kwa Familia, Mkurugenzi Mkuu, Wafanyakazi wa TBC, Waandishi wa Habari wenzangu, ndugu jamaa na marafiki wote, Mwenyezi Mungu amweke mahali pema peponi… Bwana alitoa, Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe, Amina”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.