Aliyefungwa Urusi kuzikwa Tanzania

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt Stergomena Tax amesema Mtanzania Nemes Tarimo aliyefariki Nchini Urusi alikuwa Nchini humo kwa ajili ya masomo katika chuo cha Moscow Technology Pro mwaka 2020 kabla ya kujiunga na Jeshi binafsi la Urusi la Wagner Group akiwa anatumikia sehemu ya kifungo chake cha miaka 7 kwa makosa ya kihalifu.

"Tarimo akiwa gerezani alipewa nafasi ya kujiunga na kikundi cha kijeshi cha Wagner kwa ahadi ya kulipwa fedha lakini kwa ahadi ya kuachiwa huru mara baada ya vita na umauti ulimkuta October 24,2022 na Wizara imewasiliana na Serikali ya Urusi ili kukabidhiwa mwili na ukabidhiwe kwa Familia kwa maziko, mwili umeondoka Urusi leo asubuhi"

"Nemes Tarimo alikwenda nchini Urusi mwaka 2020 kwa masomo ya shahada ya uzamili katika fani ya biashara, March 2022 alihukumiwa kifungo cha miaka saba kwa vitendo vya uhalifu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.