TFF YAMWITA FEISAL SALUM

Shirikisho la soka Tanzania (TFF) imemuandikia mchezaji Faisal Salum ‘Feitoto’ barua ya wito kwenye Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji mchezaji siku ya Ijumaa Januari 6, 2023 kwa ajili ya kusikiliza shauri lake na klabu yake ya Yanga SC.

Awali kikao hicho lilikuwa kifanyike Januari 4, 2022 lakini kwa mujibu wa ripoti kikao hicho kitafanyika siku ya Ijumaa Januari 6,2022.

Feitoto alivunja mkataba wake na klabu yake ya Yanga SC na kusafiri kwenda Falme za Kiarabu ambapo inadaiwa amekwenda kuanza majukumu yake mapya.

Feisali anatarajia kuwasili nchini kesho alfajiri akitokea Falme za Kiarabu tayari kwa kwa kikao hicho cha Ijumaa

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.