Kuhusu Pele upete anena

ANAANDIKA NAZARETH UPETE

Zitazame vyema hizo picha! Ni katika nyakati ambazo ubaguzi wa rangi ulikuwa mwepesi 'kama mchuzi wa kwale' tu! Mwanaume mweusi amebebwa na kushangiliwa na weupe... Anaombwa jezi... Ilikuwa lazima uwe si wa kawaida ili uombwe!

Anaitwa Edison Arantes Do Nascimento, dunia inamjua kama Pelé! Alizaliwa 23/10/1940 pale Três Coraçoes kwa wazazi João Ramos na Dona Celeste na walimuita zaidi 'Dico' jina ambalo mama yake alimuita mpaka uzeeni likiwa sawa na 'Tabu' au 'Kisababisha hofu'.

Jina la Pelé lilitokana na yeye kushindwa kulitamka vyema jina la mchezaji mwenza wa Baba yake Mzazi aliyeitwa Jose Lino 'Bile' aliyemtazama kama kielelezo chake yaan Role Model na Pelé alilitamka kimakosa akimuita 'Pile' au 'Pele'.

Hali hiyo ilimfanya wenzie wamcheke na waanze kumuita Pelé wakimuigiza na licha ya kulikataa sana lakini lilikua na kuzoeleka! Alishawahi kumpiga Mwanafunzi mwenzie shuleni kisa jina hilo kiasi cha kusimamishwa Shule kwa siku 2!

Akiwa na miaka 15 alionwa kipaji chake mtaani na kocha Weldemar Do Brito aliyemuombwa kwa wazazi aende naye Santos akamjaribu... Kule alipita bila kupingwa! Mwaka mmoja baadae akaingia timu ya Taifa ya Brazil na 1958 kwenye Kombe la Dunia alifunga bao akiwa na miaka 17 na siku 239 vs Wales rekodi ambayo imesogelewa 2022 na Pablo Gavi wa Spain aliyefunga akiwa na miaka 18 na siku 110 vs Costa Rica!

Alifunga Hat Trick dhidi ya Ufaransa kwenye nusu fainali na bao 2 kwenye fainali dhidi ya Sweden! Wakatwaa ndoo tena 1962 ingali yeye aliumia. Hakuwahi kusahau 1966 kwenye kombe la Dunia alipotwangwa mitama na mkong'oto wa hatari na mabeki na kupata majeraha yaliyomfikirisha kustaafu.

1970 akarudi na kutwaa ubingwa tena! Amefunga mabao 1281 kwenye mechi 1363 ingali Takwimu hizo ni za kimapokeo! Novemba 19, 1969 mbele ya mashabiki Laki 1 alifunga bao lake la 1000! Ndiye mwanadamu mwenye wastani mkubwa wa kufunga duniani akiwa na 0.92 kwa kila mechi. Alistaafu 1977.

Pele alishawahi kuwa waziri wa Michezo wa Brazil 1997 na alitajwa kuwa mwanamichezo bora wa Karne 1999 sanjari na Diego Maradona! Amefariki Dunia akiwa na miaka 82 akiwa na ushawishi mkubwa! Kiufupi sana😊

R.I.P one of the best!
Wasalaam!
CC nazareth_upete


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.