Mpole kwakheri Geita Gold

GEITA GOLD YAACHANA NA MPOLE: Klabu ya Soka ya Geita Gold imetangaza kuachana na nyota wake ambaye ni Mfungaji Bora msimu uliopita kwenye NBC Premier League, George Enock Mpole kwa makubaliano ya pande zote mbili

“Uongozi umefikia hatua hii baada ya kuzungumza na mchezaji kwa kina na kufikia maridhiano hayo kwa maslahi mapana ya klabu na mchezaji mwenyewe” sehemu ya taarifa ya klabu hiyo iliyowekwa kwenye ukurasa wao wa Instagram ya @geitagoldfc.

Kwenye msimu uliopita Mpole aliweka kambani magoli 17 kwenye NBC Premier League na kutoa pasi za mwisho (assist) tatu pamoja na kupewa kadi za njano tano.
Dirisha dogo la usajili linakuja, wape atue?



#GeitaGold #GeorgeMpole #Soka

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.