Mwalimu huyu Asihamishwe Ili Mwanafunzi Asaidiwe hapa MAKETE

Mwalimu Asihamishwe Binti huyu Asaidiwe hapa MAKETE 
Bonyeza Link hii hapo chini Ili kutazama taarifa hii.

https://youtu.be/eRa2X5dZ2f0

Maagizo ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Makete kuhusu Mwanafunzi huyu.

KWA mwenye kutaka kumsaidia binti huyu au Taasisi tuwasiliane hapa 0769771572

Katika mahafali ya kidato cha nne mwaka 2022  katika  shule ya sekondari Lupalilo iliyopo wilayani Makete mkoani Njombe  Mkuu wa shule hiyo Jones Liombo alitoa zawadi kwa wanafunzi walioweza kumsaidia mwenzao mwenye mahitaji maalumu Nesta sanga kwa kumbeba Mgongoni na kumsukuma kwenye Baiskeli ya wenye mahitaji maalumu aliyokuwa akiitumia mwanafunzi huyo.
baada ya kutoa zawadi kwa wanafunzi walioonesha upendo kwa mwenzao Mwalimi Liombo alitokwa na machozi ikiwa ni ishara ya upendo na uchungu kama mzazi kwa mwanafunzi wake Nesta sanga mwenye ndoto za kuwa mwanasheria hapo badaye.
kufuatia hali hiyo mwenyekiti wa CCM wilayani Makete mkoani Njombe clementi Mwawite ngajilo aliagiza mwalimu huyo asihamishwe ili mwanafunzi huyo aendelee kupatiwa malezi chini ya mwalimu huyo huku akisema hata akifaulu aendelee kusoma katika shule hiyo.
Baba mzazi wa Nesta sanga ndugu Fabian Mobile Sanga amemshukuru mwalimu huyo na wanafunzi wote waliomsaidia binti yake pamoja na changamoto alizopitia mwanaye.
kwa mwenye kutaka kumsaidia binti huyu au Taasisi tuwasiliane hapa 0769771572

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.