Walimu na askari Hawa kufungwa jela

serikali imeweka bayana dhamira yake ya kuwachukulia hatua kali za uwajibikaji kwa maafisa elimu wa mikoa,wilaya ,walimu na skari ambao wamepewa jukumu la kusimamia mitihani.
hatua hizo dhidi ya wasimamizi hao wa mitihani zatahusisha kuwasimamisha kazi kuwafukuza pamoja na kuwafikisha mahakamani ili wafungwe  jela.
waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Professa Adolf Mkenda ameyasema hayo leo disemba 5,2022 wakati akizungumza na uongozi wa chuo kikuu cha afya na sayansi shirikishi Muhimbili kampasi ya mlongazila katika wilaya ya Ubungo mkoani Dar es saalam alipofanya ziara ya siku moja.
"udanganyifu katika mitihani unamadhara mawili kwanza kumwezesha mtu ambaye hakustahili kuendelea na masomo badaye awe daktari pia kuwafundisha watoto wetu kuwa ili uendelee lazima uwe mdanganyifu  tunaanza kujenga corruption mapema sana,
wale waliohusika hasa watumishi wa serikali maafisa elimu na watu wote waliohusika mahali pao kwa kweli ni jela
tunaongea na mamlaka husika kwamba tusije tu kuwafukuza kazi wanachokifanya ni kitendo cha kijinai na ukiangalia gharama za kuendesha mitihani ni kubwa sana kwa hiyo mtu anayevuruga mitihani nadhani anahujumu uchumi wa nchi yetu
kwa hiyo tunaendelea kuzungumza na mamlaka kwamba watu hawa tusiwachukulie tu hatua kwa kuwafukuza kazi au kuwasimamisha kazi washitakiwe mahakamani wahukumiwe na waende jela 
tuna pitia pia sheria zetu kwamba kama kuna upenyo unaowawezesha watu wafanye udanganyifu na wa  kutoka tu bila kufanyiwa hatua yoyote tupeleke mapendekezo kwa kufanya mabadiliko ili kwa yeyote anayechezea mtihani wala asipigwe faini afungwe jela waache kufundisha watoto corruption"
amesema hilo ni onyo kwa watumisho wa serikali kwa nzia maafisa elimu wa mkoa,wilaya walimu wanaosimaamia mitihani pamoja na askari kwa kufungwa jela pindi wakibainika kufanya udanganyifu wa aina hiyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.