Fiston Mayele mchezaji bora Congo DRC

-Fiston Mayele kutwaa Tuzo ya mchezaji bora wa DR Congo ni jambo jema sana kwake,kwa Yanga na Tanzania kwa ujumla kwani inaongeza thamani ligi yetu na kuongeza wafuasi wengi zaidi..

-Lakini mimi binafsi hizi tuzo huwa naziangalia tofauti kidogo...

-Ukimuambia hata shabiki wa Yanga kwamba Mayele ni bora kuliko Yoane Wissa yule wa Lorient na huyu wa Brentford atakuambia HAPANA.

-Ispokuwa, Sisi Watanzania tuna Dunia yetu kwenye masuala ya mitandao ya kijamii na Tuzo yoyote hapa Afrika inayomhusisha mchezaji anaecheza Yanga au Simba linapokuja suala la Kura za mitandaoni ni asilimia kubwa Tuzo lazima ije Bongo.

-Haishangazi kuona picha za nyota wa Simba na Yanga zikitawala kwenye page za CAF...Tuko bora sana eneo hilo!

-Ukijumlisha idadi ya followers wa nyota wote waliokuwa wanashindania hiyo Tuzo aliyobeba Mayele (Wissa 50K,Mbokani 97K,Elia,Muleka 199K,Kebano 64K,Mbemba 177K na Mayele442 mwenyewe) hawafikii idadi ya followers wa Ali Kamwe.

-Maana yake nini..?
Ukiweka kwenye mzani unaona Wabongo wako vizuri zaidi kuwafuatilia mastar wao na wadau wa soka kuliko nchi nyingi za kiafrika.

-Na huu ndio utamaduni unaoendelea kubaki mioyoni mwa nyota kadhaa na kuwatesa Kama Adebayor,Manzoki,Bobosi na wanatamani siku moja kuja nchini Tanzania kuchezea vilabu hivi.

-Nyota wengi wamekuja hawana hata account Instagram lakini sasa Account zao ziko vyema sana na wengine wamezalisha vipato kwa baadhi ya wabongo waliotengeneza account fake na wanapata matangazo.

#NB: Huyu Mayele angeendelea kubaki As Vita halafu akashindanishwa na Kibu Denis wa Simba au Crispin Ngushi wa Yanga pengine Mayele asingeibeba!

Sambamba na uwezo wake mkubwa wa kufunga, Ukubwa wa Timu yake na hamasa ya mashabiki wa Yanga ambao ni miongoni mwa mashabiki wanaowapenda sana wachezaji wao ndio chachu ya Mayele kutwaa Tuzo na sio kwamba Mayele ni bora kuliko hao wengine wanaocheza Ulaya.

ANAANDIKA Sospeter Ilagila.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.