Mambo ya uchaguzi yameanza Simbasc

Kamati ya Uchaguzi ya Simba imeingia kwenye malalamiko makubwa kwa wale ambao imewaengua kwa kile kinachoelezwa sababu za kimaadili katika Uchaguzi wa Klabu hiyo wa Januari 29 mwaka huu.

Taarifa zinasema Kamati ya Uchaguzi Simba inataka mapingamizi ambayo yamewasilishwa na walioenguliwa ya Kimaadili iyasikilize wao kinyume na kanuni za Uchaguzi wa Simba ambazo zinataka Kamati ya Maadili ndio iyasikilize.

Miongoni mwa walioenguliwa pasipo hata kujulishwa sababu za kuondolewa japo zikielezwa juu juu kuwa ni za kimaadili ni Geofrey Nyange Kaburu aliyekuwa anaomba kuwania Uenyekiti wa Klabu hiyo.

Kaburu na wengine 11 akiwemo mwana-Mama Amina Karuma aliyekuwa anaomba kuingia Ujumbe wa Bodi ya Simba kupitia Wanawake, wamepigwa chini huku sababu hazielezwi na kesho Kamati ya Uchaguzi imepanga ijipe jukumu wao wenyewe la kusikiliza malalamiko ya hao wanaopiga kuenguliwa kitu ambacho ni kinyume na Kanuni za Uchaguzi wa Simba.

Kamati ya Maadili ya Simba inaongozwa na Charles Kenyela na wakati Kamati ya Uchaguzi inakaa kesho kusikiliza malalamiko hayo ya Kimaadili, Kamati yake haijajulishwa lolote.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.