Karume aliipa Simbasc jina

"Mapinduzi walijua watu wachache sana.
Yeye alikuwa na mipango yake na yeye ndiye aliyekuwa mkuu. Alikuwapo hapa Zanzibar. Lakini hakuniambia hata mimi kuwa kuna mapinduzi siku hiyo. Ililia risasi ya kwanza na ya pili nikamwambia unasikia risasi hizo, ndiyo akanieleza kuwa kuna mapinduzi wameyaandaa na amewatuma vijana.

Akanieleza kuhusu mpango mzima wa mapinduzi na akanipa wosia akanieleza mambo kadhaa, akasema; “Tukifanikiwa itakuwa vyema lakini tukishindwa mimi nitakuja kuchukuliwa na kunyongwa.”

"Ilipofika Saa 11: 30 Alfajiri gari ikaja ina alama yetu ya Bendera ya Kisima kwa hiyo nikawa sina wasiwasi. Yule mtu akashuka akaenda kwa nyuma akagonga mlango akimtaka Mzee Karume. Akamwambia twende 'ukatangaze Mapinduzi' Mama Fatma Karume.

#MapinduziDay

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.