Waiba alama za barabarani Makete Njombe

Watu wasiojulikana wameng'oa na kuiba Mabomba matano ya Vibao vya alama za  usalama Barabarani katika Barabara kuu ya Makete - Njombe usiku wa kuamkia January 13, 2023 katika eneo la kijiji cha Ikonda wilayani Makete mkoani Njombe

Wakizungumza na kituo hiki kwa nyakati tofauti baadhi ya wananchi, Mwalimu Elyakimu Sanga, Mchungaji Brown Luvanda pamoja na Chrispini Mhema  wamesema kuwa matendo kama hayo hayapaswi kufumbiwa macho

Wananchi hao wamesema suala la ulinzi ni la kila mwananchi hivyo washirikiane katika kuwabaini waliohusika kuhujumu miundombinu ya serikali ikiwa ni pamoja na kuhakikisha ulinzi wa mali za umma unafanyika kwa kushirikiana na mwananchi mmoja mmoja

Alexander Mbilinyi ni mwenyekiti wa kijiji cha Ikonda amewataka wananchi kutambua kuwa wote wameibiwa hivyo kwa pamoja washirikiane kuwabaini wahalifu hao

Licha ya Serikali mara kwa mara kutoa rai kwa wananchi kuacha kuiba vifaa vya ujenzi wa barabara ikiwa ni pamoja na kutunza miundombinu iliyopo, lakini wapo baadhi yao wamekuwa wakipuuza na kuendelea kuiba.

#greenfmUpdates @tanroadshq

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.