Mjamzito afumaniwa akijamiana Hospjtali

Alikuwa amelazwa kwa siku tano hospitalini na siku mumewe alipoenda kumwona, akamfuma akifanya mapenzi na kijana wa miaka 24.

Apac, Uganda. Mwanaume mmoja amemfumania mkewe aliye mjamzito akifanya mapenzi hospitalini alikokuwa amelazwa akitibiwa malaria.

Mwanamke huyo alilazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Apac kwa siku tano na fumanizi hilo lilitokea mume alipomtembelea mkewe muda wa kuona wagonjwa.

Badala ya kupokelewa na sura ya maumivu yatokanayo ya maradhi yanayomsumbua mkewe, mume huyo alimfuma mkewe akifanya kitendo hicho na kijana mdogo wa miaka 24 tu ambaye huchoma nyama mjini hapo.
Baada ya kufumaniwa, kijana huyo alikimbia wakati mume akiwa na mshangao wa alichokishuhudia lakini alikamatwa na kupelekwa kituo cha polisi ambako amefunguliwa mashtaka aliyoyakiri.

Gazeti la Daily Monitor la nchini Uganda linaripoti kuwa Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Apac, Davis Ndaula amethibitisha kushikiliwa kwa kijana huyo ambaye aliwapa shida kesi ya kumfungulia lakini baada ya kutafakari akashtakiwa kwa kusababisha kero kwa umma kwa kitendo alichokifanya katika wodi ya wanawake hospitalini hapo.

“Mume wa huyu mwanamke alikuja kumjulia hali mkewe aliyelazwa hospitalini kwa siku tano lakini akamfumania akiwa na kijana huyo wakijamiiana kwenye kitanda cha hospitali,” amesema shuhuda ambaye hakutaka kutajwa jina.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.