Stars Yaibuka na Ushidi mbele ya Uganda.


Bao la Simon Msuva (1-0) dakika ya 68 limeipa Taifa Stars πŸ‡ΉπŸ‡Ώ pointi 3 muhimu ugenini dhidi ya Uganda πŸ‡ΊπŸ‡¬ mechi ya kufuzu Afcon 2023 iliyochezwa uwanja wa Suez Canal nchini Misri.

Stars ambayo ipo kundi F inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi 4 nyuma ta Algeria yenye pointi 9 huku Niger ikishika nafasi ya tatu pointi 2 na Uganda nafasi ya mwisho pointi 1 wote wakiwa wamecheza mechi 3.

Mechi inayofuata Stars itaikaribisha Uganda uwanja wa Mkapa Machi 28.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.