KOCHA WA US MONASTIR AIPATABIRIA YANGA KUTINGA NUSU FAINALI YA KOMBE LA SHIRIKISHO.

KOCHA WA US MONASTIR  AIPATABIRIA YANGA KUTINGA NUSU FAINALI YA KOMBE LA SHIRIKISHO.

Akizungumza na Mwanaspoti, kocha wa klabu ya US Monastir amesema Yanga ina mambo mawili (2) mazuri yanayowabeba na wananafasi kubwa ya kufuzu nusu fainali iwapo watayaongezea nguvu,

"Ubora wa kwanza wa Yanga wanaoongoza kundi letu ni uwepo wa kocha Nasreddine Nabi ambaye ameiweka Yanga mahali salama kimbinu na kwamba hata ukiwa mbele unaongoza kwa bao (1) unahitaji ubora kulilinda bao lako kwa kuwa Nabi ni kocha anayebadilika badilika"

"Tulipocheza na Yanga tukashinda (2-0) lakini muda wote hatukuwa na utulivu wa kuona kama tumemaliza mechi. Nawaheshimu sana (Yanga) kwa kuwa wanaonesha kuna kazi kubwa kocha wao amefanya.. Hata nilipokuwa nawafuatilia na kuangalia mechi zao sikuona kama kuna mchezo wamezidiwa umiliki wa mpira"

"Napenda wanavyocheza, wanakulazimisha, wakati wote wanataka mpira uwe katika miliki yao. Tulipocheza nao kisha kucheza na Tp Mazembe tuliona tofauti kubwa ilitosha kuona kwamba Yanga watakuwa washindani wetu wakubwa katika kundi letu"

"Silaha ya pili ya Yanga ni wale  washambuliaji wawili kwenye eneo la mbele, yule namba 9 (Mayele) ni hatari anajua sana kufunga lakini pia anakasi. Kuna yule jezi namba 25 (Musonda) ndio tatizo zaidi, unapokuwa na washambuliaji wa namna ile wanawalazimisha mabeki kupoteza nidhamu yao kutokana na kasi yao. Kitu kibaya zaidi wanacheza kwa ushirikiano mkubwa"

"Kwangu mimi nawaona (Yanga) watafika mbali kama watabahatika katika droo kutokukutana na timu ngumu. Najiandaa kuwaona wanacheza NUSU FAINALI"

Darko Novic -Kocha mkuu wa klabu ya US Monastir

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.