TANZIA: Papa Benedict wa XVI afariki dunia

Papa Benedict wa XVI amefariki dunia leo akiwa na umri wa miaka (95), Vatican imesema itatoa taarifa zaidi kuhusu kifo chake muda mfupi ujao.
Mapema Wiki hii Papa Francis alisema Mtangulizi wake Papa Benedict XVI mwenye umri wa miaka 95 ni mgonjwa sana na akawataka Mahujaji wa Vatican wamuombee.

Papa Benedict wa XVI ndiye alikuwa Kiongozi wa kwanza wa kanisa katoliki kujiuzulu mwaka 2013 na kuushangaza Ulimwengu kwakuwa jambo hilo lilikuwa halijawahi kutokea katika kipindi cha miaka 600 iliyopita.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.